Kitengo cha kukabiliana na dharura kaskazini mwa nchi chazinduliwa

Kitengo hicho ambacho kina wanachama 229, kimejukumiwa kukabiliana na ugaidi ,wizi wa mifugo  na migogoro baina ya jamii katika eneo nzima la kaskazini mashariki mwa nchi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kitengo cha polisi kukabiliana na dharura kaskazini mwa nchi chazinduliwa.

Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat, amezindua kitengo cha polisi cha kukabiliana na dharura  (QRU), chenye makao yake Garissa.

Kitengo hicho ambacho kina wanachama 229, kimejukumiwa kukabiliana na ugaidi ,wizi wa mifugo  na migogoro baina ya jamii katika eneo nzima la kaskazini mashariki mwa nchi na nchi Jirani.

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitengo hicho Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat,  alimtawaza kamishna  wa polisi Samuel Mukuusi kuwa  Kamanda wa kwanza  wa kitengo hicho.

“Tumekuja Garissa leo kuzindua kitengo cha Quick Response Unit (QRU), ambacho kinakuja kushughulikia maswala ya kiusalama katika maeneo kadhaa ya nchi hususan Garissa, Isiolo, Laikipia, Samburu na Mandera,” alisema Lagat.

Lagat aliagiza kitengo hicho kushirikiana kwa karibu na  vitengo vingine vya kiusalama, kuziba mianya ya  utekelezaji inayotumiwa na  magenge ya uhalifu

Huku wakiahidi  usaidizi endelevu wa vifaa vya kisasa na mafunzo  Lagat alitoa changamoto kwa Kamanda wa kitengo hicho Mukuusi kudumisha nidhami,uwajibikaji na kuheshimu haki za kibinadamu,akiwakumbusha maafiaa kuwa oparesheni kali ya kimkakati  lazima itekelezwe kwa kuzingatia sheria.

“Hatua hi itaboresha hali ya usalama katika mipaka ya Garissa na Isiolo, ambako kumekuwa na ghasia za kijamii zilizosababisha maafa,” aliongeza Lagat.

Share This Article