Masomo ya vyuo vikuu vya umma kurejelewa Jumatatu baada ya kumalizika kwa mgomo

Mgomo huo ulimalizika baada ya serikali kuafikiana na UASU kulipa shilingi bilioni 20 katika kipindi cha miaka mitatu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Masomo katika vyuo vyote vikuu vya umma yanatarajiwa kurejelewa Jumatatu ijayo Novemba 2, kufuatia kumalizika kwa mgomo wa kitaifa uliodumu kwa kipindi cha wiki  nne zilizopotea wakati wa mgomo wa wahadhiri.

Vyama vya wahadhiri na  wafanyakazi wa vyuo vikuu viliafikia wiki siku ya Ijumaa kumaliza mgomo wa kitaifa uliodumu kwa kipindo cha wiki nne.

Hata hivyo huenda wahadhiri watafute mbinu ya kuongeza muhula wa masomo kwa wanafunzi au njia ya kufidia muda ulioptea wakati wa mgomo.

Mgomo huo ulimalizika baada ya serikali kuafikiana na UASU kulipa shilingi bilioni 20 katika kipindi cha miaka mitatu.

Katika awamu ya kwanza  ya mwaka wa kifedha wa mwaka 202/2027 serikali itatoa shilingi bilioni 6.7, na kiwango sawia katika mwaka wa kifedha wa mwaka 2027/2028, huku awamu ya mwisho ya shilingi bilioni 6.6, ikitolewa mwaka 2028/2029.

Wahadhiri watapokea nyongeza ya asilimia 3.5 na nyongeza ya shilingi  18,000 kama marupurupu ya usafiri.

 

 

Share This Article