Serikali yakosoa Saudi Arabia kuwawekea Wakenya vikwazo vya usafiri

Duale alisema watu wote  135 waliotanagamana na mwathiriwa wa kwanza wa ugonjwa huo walitambuliwa, na 118 kati yao waliwekwa karantini,

Tom Mathinji
1 Min Read
Aden Duale - Waziri wa Afya.

Serikali ya Kenya imelalamikia hatua ya Saudi Arabia ya kuwawekea Wakenya vikwazo vya usafiri, kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Kupitia kwa taarifa siku ya Jumamosi, Waziri wa Afya Aden Duale, alitaja hatua hiyo kuwa yenye nguvu zaidi na isiyoambatana na hali ya maambukizi ya ugonjwa huo nchini Kenya.

Duale alisema kuwa serikali ilifanikiwa kudhitibi ugonjwa huo, na hakuna ushahidi kwamba umeenea kwenye jamii, akikariri kuwa hakuna maambukizi mapya tangu Oktoba 19, 2026.

“Wizara ya Afya nchini Kenya imefahamu kwa mshangao hatua kali zilizochukuliwa na Saudi Arabia kuhusiana na mlipuko wa Ebola nchini Kenya,” alisema Duale kwenye taarifa hiyo.

Waziri huyo alisema watu wote  135 waliotanagamana na mwathiriwa wa kwanza wa ugonjwa huo, walitambuliwa, na 118 kati yao waliwekwa karantini, huku maafisa wa afya wakiendelea kukabiliana na ugonjwa huo.

Aidha, Duale alisema visa vyote nane vya ugonjwa wa Ebola vilivyothibitishwa, vilihusishwa moja kwa moja na mgonjwa wa kwanza. Visa hivyo vinajumuisha wahudumu wanne wa afya na wanafamilia wanne wa karibu na mgonjwa wa kwanza.

Share This Article