Mfanyabiashara mmoja kutoka jijini Kampala nchini Uganda, ambaye alighushi saini ya Rais Yoweri Museveni amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela.
Alifanya hivyo ili kushinikiza kuongezwa kwa mkataba wenye faida kubwa wa kivuko cha serikali.
Nicholus Male alipatikana na hatia na Mahakama ya Hakimu Mkuu ya Buganda Road mnamo Oktoba 19, 2026, baada ya kukiri mashtaka saba ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo.
Mahakama ilimhukumu kifungo cha miezi 18 kwa kila shtaka, huku vifungo hivyo vikiendeshwa kwa wakati mmoja. Hii ina maana kwamba atatumikia kifungo cha miezi 18 badala ya jumla ya miaka 10 unusu.
Kwa mujibu wa Kitengo cha Kupambana na Ufisadi cha Ikulu ya Rais nchini Uganda, Male alighushi nyaraka za rais ili kushawishi kuongezwa kwa mkataba wa kampuni ya Nation Oil Distributors Limited wa kusimamia kivuko cha MV Kalangala kinachomilikiwa na serikali.
Kivuko hicho huhudumia abiria katika njia ya usafiri kati ya Entebbe na Kalangala.