Oparanya, viongozi wa Magharibi wapanga mikakati kuelekea 2027

Martin Mwanje
1 Min Read

Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya amekutana na viongozi wa eneo la Magharibi kujadili mustakabali wa eneo hilo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. 

Oparanya anasema wakati wa mkutano huo, walijadili vipaumbele vya ustawi wa kikanda, fursa za kiuchumi na maslahi ya pamoja ya watu wao.

“Mazungumzo yetu yalisisitiza umuhimu wa umoja, uongozi wenye dhamira na ushirikiano wa karibu katika kuendeleza ajenda ya pamoja ya kikanda,” alisema Oparanya ambaye wakati mmoja alihudumu kama Gavana wa Kakamega.

“Tuliangazia namna eneo la Magharibi linaweza kutumia uwezo wa idadi kubwa ya watu wake, kilimo na kiuchumi, kupanua fursa na kuimarisha ushawishi na usemi wa kisiasa wa kanda hiyo katika kutoa mwelekeo wa maendeleo ya nchi.”

Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa amenukuliwa akitaka Oparanya kutimuliwa serikalini kwa madai ya kuhujumu utendaji kazi wake.

Share This Article