Tanzania imetangaza azma ya kufufua marekebisho ya katiba, huku juhudi za maridhiano ya kitaifa zikiendelea.
Rais Samia Suluhu Hassan, alisema haya siku ya Alhamisi alipokutana na viongozi kutoka vyama vinane vya kisiasa.
Aliongeza kuwa mchakato wa maridhiano na uwiano kisiwani Zanzibar, unaendelea vyem huku ukikaribia kukamilika.
Samia aliahidi kuwa ataendelea kufanya mikutano kila baada ya miezi mitatu na viongozi wa vyama vya upinzani.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wenyeviti pamoja na manaibu wa vyama vya kisiasa.