Waziri Murkomen atua Italia kuimarisha uhusiano wa usalama

Martin Mwanje
2 Min Read

Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amewasili jijini Roma nchini Italia ambako anatarajiwa kufanya mikutano ya ngazi ya juu ya usalama. 

Wakati wa ziara hiyo, Murkomen anatarajiwa kufanya mazungumzo na Waziri wa Usalama wa Italia Matteo Piantedosi na maafisa wakuu wa asasi mbalimbali za usalama za nchi hiyio.

Pia anatarajiwa kutia saini makubaliabo ya ushirikiano kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika usimamizi wa uhamaji na usalama wa kimataifa.

Murkomen anaitembelea Italia miezi mitano baada ya mwenyeji wake, Waziri Piantedosi, kutembelea Nairobi mwezi Julai mwaka huu.

Wakati wa ziara hiyo, Kenya na Italia zilitia saini Barua ya Dhamira kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika kuzuia na kukabiliana na uhalifu wakati ushirikiano wa usalama kati ya nchi hizo mbili ukizidi kuongezeka.

Barua hiyo ya Dhamira inatoa mpangokazi wa kuhamasisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na mamlaka za polisi za nchi hizo, ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kupangwa wa kimataifa.

“Kenya inakaribisha mbinu iliyounganishwa inayotambua uhusiano thabiti kati ya maendeleo, usimamizi wa uhamiaji, na usalama,” alisema Murkomen wakati wa utiaji saini barua hiyo wakati huo.

Chini ya makubaliano hayo, pande hizo mbili zilikubaliana kutenga vituo vya mawasiliano ili kuunga mkono mipango na shughuli za ushirikiano wa kimkakati katika ngazi za pande mbili na nyingi.

Share This Article