Kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Africa (CDC), kimesema kuwa ugonjwa wa Ebola bado haujadhibitiwa miezi sita baada ya kuzuka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Jean Kaseya, amesema iwapo msambao wa ugonjwa huo hautasitishwa, basi huu utakuwa mlipuko mkubwa zaidi wa Ebola kote duniani.
“Iwapo hautazuia ueneaji, huu utakuwa mlipuko mkubwa zaidi wa Ebola kote duniani,” alisema Kaseya.
Tangu mlipuko wa Ebola utangazwe Mei 15,2026, watu zaidi ya 11,200 wameambukizwa, huku vifo 5,500 vikinakiliwa kutokana na makali ya ugonjwa huo, kulingana na takwimu za serikali ya DRC.
Kulingana na Kaseya, zaidi ya asilimi 80 ya visa vipya, vimetoka nje ya waliotangamana na waathiriwa, na zaidi ya asilimia 65 ya vifo vimetokea nje ya vituo vya matibabu.
Mataifa kadhaa ya Mashariki, Magharibi na kati kati mwa Afrika yamenakili visa vya maambukizi ya Ebola, huu ukitajwa msambao mkubwa zaidi wa Ebola kuwahi nakiliwa.