Kenya imechaguliwa tena kwenye Baraza la Chama cha kimataifa Mawasiliano ya Simu (ITU) kwa kipindi kipya cha miaka minne, baada ya kupata kura 136 kati ya kura 173 zilizopigwa.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali William Kabogo, alitangaza hayo baada ya mkutano wa ITU ulioandaliwa Doha, Qatar, ambapo Kenya ilipata nafasi kwenye baraza hilo kwa muhula wa mwaka 2027-2030.
Kenya ilikuwa miongoni mwa mataifa 19 ya Afrika, yaliyowania viti 13 vilivyotengewa bara hilo.
Côte d’Ivoire iliibuka ya pili kwa kura 135, Senegal ilipata 134 huku Tanzania ikirithika na kura 131, kulingana na matokeo rasmi ya uchaguzi huo.
Kulingana na Kabogo, jukumu hilo jipya litatoa fursa kwa Kenya kuendelea kutoa mchango wake kwa uongozi wa chama hicho, ikiwa ni pamoja na utoaji maamuzi kuhusu mpango wa kifedha wa mwaka 2028–2031.
“Katika baraza hilo, Kenya itashinikiza uunganishaji nafuu, ujuzi wa kidijitali, uaminifu kwenye huduma za dijitali na sauti dhabiti ya Afrika kuhusu sera za Kimataifa za ICT,” alisema Kabogo.