Mkenya Agnes Jebet Ngetich alitwaa medali ya dhahabu huku akiweka rekodi mpya ya dunia ya nusu marathoni katika siku ya mwisho ya mbio za barabara duniani mjini Copenhagen,Denmark.
Ng’etich aliye na umri wa miaka 25 aliziparakasa mbio hizo kwa muda wa lisaa moja dakika 5 na sekunde 15,akivunja rekodi ya Mkenya mwenza Peres Jepchoirchir ya muda wa lisaa limoja dakika 5 na sekunde 16 ya mwaka 2020.
Veronica Loleo pia wa Kenya alishinda fedha kwa lisaa limoja dakika 6 na sekunde 5,huku shaba ikitwaliwa na Florence Niyonkuru wa Burundi, sekunde tano mbele ya Daisilah Jerono kutoka Kenya aliyechukua nafasi ya nne.
Kenya ilinyakua taji ya timu ikifuatwa na Marekani na Ethiopia, katika nafasi za pili na tatu mtawalia.
Mswidi Andreas Almagren alishinda mbio za wanaume kwa dakika 58 ma sekunde 6 akifuatwa na Nicholas Kipkorir wa Kenya aliyenyakua fedha kwa dakika 58 na sekudne 11 wakati Joshua Cheptegei wa Uganda akiambulia shaba.
Kenya pia ilinyakua taji ya timu katika mbio za wanaume.