Mechi za mzunguko wa kwanza Kombe la Dunia kukamilika leo usiku

Mabingwa mara nne wa Afrika, Ghana watakuwa uwanjani Toronto, Canada dhidi ya Panama ya Amerika Kaskazini kuanzia saa nane usiku katika kundi L.

Dismas Otuke
2 Min Read

Mechi nne za makundi za kuhitimisha mzunguko wa kwanza hatua ya makundi zitachezwa leo Jumatano usiku huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Ghana zikiwa wawakilishi wa mwisho wa Afrika kujimwaya uwanjani.

Mabingwa mara nne wa Afrika Ghana watakuwa uwanjani Toronto, Canada dhidi ya Panama ya Amerika Kaskazini kuanzia saa nane usiku katika kundi L.

Katika mchuano wa kwanza wa siku, Chui  wa DRC wanaorejea katika Kombe la Dunia baada ya miaka 54, watakabiliana na Ureno mjini Houston nchini Marekani kuanzia saa mbili usiku katika kundi K.

Tayari wawakilishi wanane wa Afrika wamesajili matokeo mseto katika mechi za mzungo wa kwanza, Ivoryu Coast ikiwa timu pekee iliyosajili ushindi baada ya kuwalaza Ecuador bao moja kwa bila kundini E.

Atlas Lions ya Morocco ilisajili sare ya bao moja dhidi ya Brazil kundini B wakati Misri pia wakipata sare iyo hiyo dhidi ya Ubelgiji katika kundi G, nao limbukeni Cape Verde wakalazimisha sare kappa dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Uhispania katika kundi H.

Hata hivyo, Afrika Kusini walibanwa goli moja kwa bila kundini A na  Mexico,  Tunisia wakaambulia kichapo cha  mabao 5-1 kutoka kwa Uswidi katika kundi F, nao Senegal wakagaragazwa magoli 3-1 na Ufaransa kwenye kundi I.

Mechi nyingine ya leo itakuw ya kundi L kuanzia saa tano usiku kati ya Uingereza na Croatia.

Share This Article