Visa vya maambukizi yay ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), vinazidi kuongeza, ambapo tayari watu 782 wameambukizwa na wengine 178 wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa huo.
Wizara ya afya ya DRC, ilidokeza kuwa visa vipya 72, vifo 29 vimenakiliwa katika muda wa saa 24 zilizopita.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia Magonjwa (Africa CDC), Jean Kaseya ametoa wito wa dharura kwa washirika na wafadhili wa kimataifa kutoa raslimali za kufanikisha kudhibiti msambao wa ugonjwa huo na kuokoa maisha.
“Tumejitolea kuzisaidia nchi ambazo zimeathiriwa na maambukizi ya ugonjwa huo, hadi msambao huo utakapositishwa. Tunatoa wito kwa washirika na wafadhili kutoa rasilimali ili kuimarisha juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo na kuokoa maisha,” alisema Kaseya.
Hadi kufika sasa hakuna tiba au chanjo iliyothibitishwa ya kukabiliana na virusi vya Ebola vya aina ya Bundibugyo.
Maaafa yanayotokana na ugonjwa huo ni asilimia 22.8, huku wagonjwa 40 wakipona ugonjwa huo kulingana na maafisa.
Mkoa wa Ituri Mashariki ndio umeathirika zaidi,ukinakili takriban asilimia 95 ya visa vilivyothibitishwa nchini DRC hadi sasa.