Klabu ya Gor Mahia, huenda itawazwe mabingwa wa ligi kuu Kenya kwa mara ya 22, mwishoni mwa juma hili endapo wataishinda Muranga Seal, siku ya Jumapili.
Zikisalia mechi tatu msimu ukamilike Gor wana alama 65, huku wapinzania wa karibu AFC Leopards wakiwa katika nafasi ya pili kwa alama 56.
Hata hivyo Gor wana tofauti ya magoli 10 zaidi ya Leopards.
Hali hii ina maana kuwa Gor, wakipata ushindi dhidi ya Murang’a Seal, watatawazwa mabingwa bila kuzingatia matokeo ya Leopards.
Leopards watacheza ugenini Jumamosi dhidi ya Kakamega Homeboyz, mechi ambayo ni sharti washinde ili kuwafanya Gor, kusubiri kutawazwa mabingwa.