Jaji Mohammed Warsame aapishwa kuwa jaji wa Mahakama ya Upeo

Dismas Otuke
1 Min Read

Jaji Mohammed Abdullahi Warsame, ameapishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Upeo katika hafla iliyoshuhudiwa na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi.

Rais amempongeza Jaji Warsame kwa kuteuliwa kuwa jaji wa 14 wa Mahakama ya upeo.

Akizungumza baada ya uapisho huo, Rais alisema ana imani na tajiriba ya jaji Warsame, ya kubadilisha na kuboresha utendakazi wa mahakama ya Upeo .

Rais pia alishuhudia uapisho wa mawakili Evans na Jedidiah Waruhiu, waliopandishwa cheo .

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Naibu Rais prof. Kithure Kindiki na Rais wa Mahakama ya Upeo Martha Koome.

Share This Article