Mashindano ya kombe la Mashuja Dei yazinduliwa

Murkomen amesema lengo la mashindano hayo ni kuleta pamoja vijana wa kaunti hizo na kuhimiza amani na kupeleka sherehe za Mashujaa karibu na wananchi walio mashinani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kaunti za Uasin Gishu,Nandi na  Elgeyo Marakwet kwa pamoja zimezindua mashindano ya michezo ya kuadhimisha siku kuu ya Mashujaa  tarehe 20 mwezi ujao.

Mashindano hayo yatafikia kilele Oktoba 20 punde  baada ya sherehe za mwaka huu za Mashujaa zilizoratibiwa kuandaliwa na kaunti hizo kwa pamoja.

Waziri wa sualama wa kitaifa Kipchumba Murkomen ameongoza uzinduzi wa mashindano  hayo yatakayowaleta pamoja viajana watakaoshindana katika fani ya Voliboli,soka,Riadha,Mpira wa Kikapu.

Murkomen amesema lengo la mashindano hayo ni kuleta pamoja vijana wa kaunti hizo na kuhimiza amani na kupeleka sherehe za Mashujaa karibu na wananchi walio mashinani.

Mashindnao hayo yataanzia ngazi ya Wadi tarehe 26 mwezi huu kabla ya kuelekea kwa yale baina ya kaunti  Oktoba 19, kwa fainali ya Voliboli  nayo fainali ya soka ipigwe Oktoba 2o.

Mbio za Iten Marathon  zitafanyika tarehe 18 mwezi ujao  huku kitita cha shilingi milioni 63 zikishindaniwa .

Hafla ilihudhuriwa na Magava wa kaunti hizo tatu wakiwa;Jonathan Bii wa Uasin Gishu, Wisley Rotich wa Elgeyo Marakwet na Stephen Sang wa Nandi pamoja na Wabunge Gladys Boss Sholei, Julius Melly, Joses Lelmengit, Paul Biego, Timothy Kipchumba, Phyllis Bartoo, Maryanne Kitany, Adams Kipsanai, Julius Rutto, Janet Sitienei na Gideon Kimaiyo.

Share This Article