Rais Ruto asaini miswada miwili kuwa sheria katika Ikulu ya Eldoret

Rais pia amesaini mswada wa marekebisho ya huduma ya kaunti wa mwaka 2023 kuhusu usimamizi wa mabunge ya kaunti.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ametia saini miswada miwili ikiwemo ule wa kuongeza mgao wa fedha za kaunti nchini kwa shilingi milioni 425.6, mapema Jumatatu katika Ikulu ya Eldoret.

Msuada huo utashuhudiwa kuongezwa kwa mgao wa pesa katunti katika kipindi cha matumizi ya fedha ya mwaka 2026-2027, hadi shilingi bilioni 71.09.

Rais amesema sheria hiyo itawezesha upatikanaji wa fedha za kufadhili afya,kilimo ,mabadiliko ya tabianchi,kiangazi miongoni mwa miradi mingine.

Aliongeza kuwa pesa hizo zimetolewa katika pato la serikali kuu ,na mikopo pamoja na ruzuku kutoka kwa washirika wa kimaendeleo wa Keny,a na kila kaunti itapata mgao sawia.

Rais pia amesaini mswada wa marekebisho ya huduma ya kaunti wa mwaka 2023 kuhusu usimamizi wa mabunge ya kaunti.

Mswada huo unafafanua kuhusu kuondolewa kwa wafanyakazi wa bodi ya kaunti na pia kupigwa marufuku au kutimuliwa kwa makarani wa mabunge ya kaunti.

Share This Article