Bien afichua orodha ya nyimbo za albamu yake ijayo

Huu ndio mradi wake mkubwa wa kwanza chini ya ushirikiano wake mpya wa kimataifa na kampuni kubwa ya muziki ya Quality Control Music.

Marion Bosire
2 Min Read

Msanii nyota wa muziki nchini Kenya, Bien, amefichua rasmi orodha ya nyimbo zitakazopatikana katika albamu yake mpya ya studio ijayo, aliyoipa jina la “Alusa Continua”.

Aliweka orodha hiyo ya albamu kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii na kundika, “Novemba 20 Tuko live. Nimeweka moyo wangu wote na nafsi kwenye mradi huu, nasubiri kwa hamu kuushiriki nanyi”.

Mojawapo ya nyimbo kwenye orodha hiyo ni “I’ll Be Okay” wimbo ambao alitoa hivi maajuzi na tayari umevutia mashabiki wake wengi ulimwenguni kote.

Nyingine ni pamoja na Alusa Continua, All my enemies are suffering, Xoxo aliomhusisha Ywaya Tajiri, Omoka, P.O Box Kakamega na Kaumbete alioimba na Costa Ojwang, jumla ikiwa ni nyimbo 17.

Albamu hiyo inatarajiwa kutolewa duniani kote Novemba 20, 2026, ikiwa ni mradi wake mkubwa wa kwanza chini ya ushirikiano wake mpya wa kimataifa na kampuni kubwa ya muziki ya Quality Control Music.

Baada ya mafanikio makubwa ya kimataifa ya wimbo wake Finale, aliomshirikisha Alikiba na ambao tayari umetazamwa zaidi ya mara milioni 61, albamu hiyo inatarajiwa kuimarisha zaidi nafasi ya Bien katika muziki wa Afrobeats duniani.

Mashabiki wanaweza kujisajili mapema ili kuhifadhi albamu hiyo kwenye majukwaa mbalimbali ya kusikiliza muziki kabla ya kutolewa kwake Novemba.

Hii hapa orodha nzima;

Share This Article