Polisi wawakamata washukiwa watano kwenye vita dhidi ya mihadarati

Tom Mathinji
2 Min Read
Washukiwa watano wakamatwa kwenye msako dhidi ya mihadarati.

Maafisa wa usalama wamewakamata washukiwa watano wa ulanguzi wa mihadari katika kaunti ya Busia.

Baada ya kupokea habari za kijasusi, maafisa kutoka kitengo cha uchunguzi wa mihadarati (NANIB), walifanya msako katika kituo cha mabasi na kumnasa Abubakar Omar Rajab, muda mfupi kabla hajaabiri basi kuelekea Jijini Nairobi.

Maafisa hao walipekua mkoba wake na kupata bangi kwenyw mfuko wa manajano, na kumpeleka mshukiwa huyo aktika kituo cha polisi cha Busia kuhojiwa.

Katika kaunti ya Homa Bay, operesheni dhidi ya mihadarati ililenga kituo cha kibiashara cha Rodi , ambako maafisa wa polisi walivamia nyumba ya makazi inayoshukiwa kuhifadhi dawa za kulevya. Msamo huo ulisababisha kupatikana kwa vipande 64 vya bandi, huku mshukiwa Elijah Ochieng Alfred akikamatwa.

Msako huo dhidi ya mihadarati kisha ulifululiza hadi kaunti ya Kitui, ambako maafisa kutoka asasi mbalimbali waliokuwa kwenye kiuizi cha barabarani kwenye Barabara Kuu ya Thika–Garissa, waliponasa mzigo uliokuwa na bangi.

Maafisa hao walilisimamisha basi lililokuwa likisafiri kutoka Nairobi kuelekea Mwingi na kuanza kuwapekua abiria.

Upekuzi huo ulisababisha kukamatwa kwa Nicholas Mathumbi Kitati, ambaye alikuwa na vipande 325 vya bangi kwenye koti lake. Mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kanyonyoo.

Katika kaunti ya Murang’a, maafisa kutoka kituo cha polisi cha Kigumo, walimwandama Evans Karanja Mwaura katika eneo la Kangari, na baada ya kupekua gari lake aina ya Toyota Fielder, walipata vipande 150 vya bangi, mshukiwa huyo anazuiliwa huku uchunguzi ukiendelea.

Vita hivyo vilielekezwa hadi kaunti ya Wajir, ambako Abdnasir Jelle alikamatwa akiwa na makasha 10 yliyokuwa na bangi. Jelle anazuiliwa kwenye korokoro za polisi uchunguzi ukiendelea.

TAGGED:
Share This Article