Shabana FC wamenza vyema msimu wa mwaka 2026 na 2027 wa Ligi Kuu ya Kenya baada ya kusajili ushindi wa bao moja kwa bila ugenini dhidi ya Posta Rangers .
Mechi hiyo ya Jumamosi katika uwanja wa Wang’uru ilishuhudia wenyeji wakipatwa na pigo baada ya mchezaji wao kulishwa kadi nyekundu kunako dakika ya 10.
Shabana walipata bao pekee na la suhindi kupitia kwa tobwe la Abdul Hafiz kunako dakika ya 68.
Katika mechi ya kufungua ligi Mathare United na APS Bomet walitoka sare tasa katika uchanjaa wa Police Sacco .
Mechi nne zaidi kusakatwa Jumapili.