Mahakama ya CAS Kuanza kusikiza rufaa ya AFCON 2025 wiki ijayo

CAS yenye makao yake mjini Laussane, Uswizi, itaanza kusikiza kesi hiyo Oktoba 8, ingawa itafanya vikao vyake kisiri.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama ya Kimataifa ya Kutatua Migogoro Michezoni (CAS) itaanza kusikiza rufaa iliyowasilishwa na Shirikisho la Soka nchini Senegal (FSF) dhidi ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF).

FSF inapinga hatua ya kamati ya rufaa ya CAF kuwapokonya kombe la AFCON na badala yake kuwatangaza Morocco kuwa mabingwa.

CAS yenye makao yake mjini Laussane, Uswizi, itaanza kusikiza kesi hiyo Oktoba 8, ingawa itafanya vikao vyake kisiri.

Aidha, CAS haijaweka bayana muda itakaochukua kusikiza na kutoa uamuzi kuhusu kesi hiyo.

Wawakilishi  wa FSF, FRMF watakuwa Uswizi wakati wote wa kusikizwa kwa kesi hiyo huku CAF ikiwakilishwa na mawakili wake.

Senegal, licha ya kuishnda Morocco bao moja kwa bila katika fainali ya mapema mwaka huu wakiwa nyumbani, walipokonywa taji baada ya kuondoka uwanjani kupinga penalti  ya dakika za mwisho iliyokabidhiwa wenyeji.

Share This Article