Kenya yaiparuza Tanzania 4-1,chipukizi chini ya miaka 23

Mechi ya marudio itaandaliwa Oktoba 10 katika uwanja wa Uhuru huku mshindi akiweka miadi ya kumenyana na Ivory Coast katika raundi ya pili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya soka kwa wanaume chini ya umri wa miaka 23 imewacharaza Tanzania mabao 4-1, katika mkondo wa kwanza wa raundi ya kwan za kufuzu fainali za AFCON mwaka ujao katika mchuano uliosakatwa kiwarani Nyayo.

Paul Osama alipachika goli la kwanza kunako dakika ya kwanza kabla ya Lawrence Okoth, kutanua uongozi kwa bao la pili dakika ya mwisho kabla ya mapumziko.

Kevin Wanganya na Kelly Madada waliongeza moja kila mmoja dakiuka za 50 na 75 mtawalia wakati  wageni Tanzania wakikomboa moja kupitia kwa mkwaju wa penati.

Mechi ya marudio itaandaliwa Oktoba 10 katika uwanja wa Uhuru huku mshindi akiweka miadi ya kumenyana na Ivory Coast katika raundi ya pili.

Mshindi wa raundi ya pili atafuzu kwa fainali za AFCON mwaka ujao nchini Misri ,mashindano ambayo pia yatakuwa ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki mwaka 2028 nchini Marekani.

Share This Article