Wakimbizi walio nchini Afrika Kusini wanahofia maisha yao huku siku ya mwisho ya Septemba 30 kwa raia wa kigeni kuhama ikikariobia.
Wengi wa Wakimbizi na raia wa kigeni tayari wamehama na kusaidiwa na serikali zao kurejea manyumbani.
Raia wa Afrika Kusini walifanya maandamano mwezi Machi mwaka huu walifanya maandamano ya kutaka watu wote kutoka nje ya nchi wasio na vibali vya kuishi na kufanya kazi wahame .
Watu kadhaa walijeruhiwa na wengine kuawa kwenye maandamano na mashambulizi yaliyotekelezwa na raia.
Baadhi ya raia wa kigeni wamekuwa wakiishi nje au kwenye mahema na kambi maalum kwa kuhofiwa kushambuliwa na wenyeji.
Wengine walipoteza mali yao iliyotwaliwa na wenyeji .