Aliyekuwa Mama wa Taifa wa Ghana Nana Konadu Rawlings amefariki

Tom Mathinji
1 Min Read
Nana Konadu Agyeman-Rawlings ameaga dunia.

Mama wa Taifa wa zamani wa Ghana Nana Konadu Agyeman-Rawlings ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 76.

Konadu aliyekuwa mjane wa Rais wa Ghana aliyehudumu kwa muda mrefu Jerry John Rawlings, alifariki Alhamisi asubuhi akipokea matibabu katika hospitali ya Ridge, jijini Accra.

Familia yake ilimtembelea Rais wa Ghana John Mahama Alhamisi alasiri kumfahamisha rasmi kuhusu kifo cha Konadu.

Nana Konadu Agyeman-Rawlings alikuwa mama wa taifa wa kwanza kutoka Juni 4, 1979, hadi Septemba 24, 1979, chini ya Baraza la Mapinduzi la Wanajeshi (AFRC), na tena kutoka Desemba 31, 1981, hadi Januari 6, 1993, chini ya Baraza la Ulinzi la Kitaifa (PNDC).

Aidha aliendelea kuhudumu wadhifa wa Mama Taifa   kutoka Januari 7, 1993, hadi Januari 6, 2001, na kutamatisha muda wa mihula miwili chini mfumo mpya wa demokrasia wa kaunti.

Ujumbe wa salamu za rambirambi unaendelea kutumwa kwa haraka katika mitandao ya kijamii kufuatia taarifa za kifo chake.

Website |  + posts
Share This Article