Rais William Ruto amefanyia mabadiliko vikosi vya jeshi akifanya uteuzi mpya wa jeshi la wanamaji, wanahewa na wa nchi kavu.
Kwenye mabadiliko hayo, Meja Jenerali David Kipkemboi Ketter amepandishwa hadi cheo cha Luteni Jenerali na kuwa Kamanda mpya wa jeshi la wanamaji, akichukua nafasi ya Luteni Jenerali David Kimaiyo Chemwaina, ambaye ameteuliwa kuwa Chansela wa chuo kikuu cha kitaifa cha wanajeshi (NDU-K).
Meja Jenerali Benard Waliaula ameteuliwa Kamanda wa jeshi la wanahewa akichukua nafasi ya Meja Jenerali Fatuma Gaiti Ahmed, ambaye muda wake kuhudumu kwa miongo minne umekamilika.
Brigedia Joel Muriungi M’arimi amepandishwa cheo hadi wadhfa wa meja Jenerali na kuteuliwa kuwa Kamanda wa Chup cha wanajeshi nchini Kenya Military Academy.
Brigedia Joyce Chelang’at Sitienei amepewa hadhi ya Meja Jenerali na atakuwa Naibu Chansela wa chuo kikuu cha NDU-K.