Waziri wa Ulinzi nchini Mali Jenerali Sadio Camara, aliuawa Jumamosi kufuatia mashambulizi yaliyotekelezwa katika kambi za kijeshi nchini humo.
Habari za kuuawa kwa Camara zilifuatia shambulizi la wanamgambo wanaohusiana na kundi haramu la Al Qaeda na waasi wa Tuaregs lililotekelezwa nyumbani kwake.
Camara alichangia pakubwa kwenye mapinduzi ya serikali na jeshi ya mwaka 2020 na 2021.
Inaaminika kuwa waasi hao walishambulia kwa mabomu nyumbani kwa Camara karibu na Jiji kuu la nchi hiyo Bamako.
Shambulizi hilo lilisababisha kuporomoka kwa nyumba ya Camara, na kuharibiwa kwa msikiti uliokuwa karibu, ambapo waumini kadhaa pia waliuawa.