Kenya yavuliwa ubingwa wa Voliboli Afrika,yakosa kufuzu Olimpiki

Kenya waliokuwa na makosa mengi walishindwa kwa seti za 22-25,15-25 na 15-25 na  15-25.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya mpira wa wavu kwa wanawake -Malkia Strikers ilishindwa kwenye fainali ya kombe la Afrika, baada ya kucharazwa seti 3-0 na Misri kwenye fainali ya Ijumaa usiku uwanjani Kasarani.

Kenya waliokuwa na makosa mengi walishindwa kwa seti za 22-25,15-25 na 15-25 na  15-25, na kushindwa kutetea taji hiyo ya Afrika waliyokuwa wamenyakua miaka miwili iliyopita.

Aidha,Kenya walikosa kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028, kufuatia kushindwa huko.

Mashindano hayo yalishirikisha timu 15 kutoka barani Afrika baada ya kujiondoa kwa Morocco.

Share This Article