Mabingwa wa Dunia na Olimpiki Emmanuel Wanyonyi na Faith Cherotich walitawazwa mabingwa wa Diamond League katika siku ya kwanza ya mkondo wa mwisho wa Brussels nchini Ubelgiji Ijumaa usiku.
Wanyonyi alishinda mbio za mita 800 akiweka rekodi mpya ya dakika 1 sekunde 41.80,mbele ya Djamel Sedjaati wa Algeria, aliyemaliza wa pili huku Yanis Mezziane wa Ufaransa akichukua nafasi ya tatu.
Cherotich pia alishinda mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji akizioparakasa kwa muda wa dakika 8 sekunde 51.61,akiweka pia rekodi moya ya mashindano.

Mkenya mwenza Doris Lemngole alichukua nafasi ya pili kwa dakika 8 sekunde 52.86 huku Winfred Yavi wa Bahrain akiambulia nafasi ya tatu.