Rais Ruto awaomboleza walioangamia kwenye ajali ya Salama

Kiongozi wa taifa aliwatakia uponyaji wa haraka, wale waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo ambao wanapokea matibabu.

Tom Mathinji
1 Min Read
William Ruto - Rais wa Kenya.

Rais William Ruto amewaomboleza mahujaji 17 wa kanisa katoliki waliofariki kwenye ajali ya barabarani katika eneo la Salama, kaunti ya Makueni Jumamosi asubuhi.

Mahujaji hao kutoka kanisa la St. Mathias Mulumba, Parokia ya Mikindani, walikuwa wakielekea katika madhabahu ya Subukia kaunti ya Nakuru, kuhudhuria maombi ya kitaifa.

“Natuma rambirambi kwa familia, marafiki, wanaparokia na jamii nzima ya kanisa katoliki, wanaoomboleza maafa hayo kwa uchungu mwingi,” alisema Rais Ruto kupitia kwa taarifa.

“Tunasimama nao wakati huu mgumu wa majonzi, tukimuomba Mungu awape nguvu, faraja na amani,” aliongeza Rais Ruto.

Wakati huo huo kiongozi wa taifa aliwatakia uponyaji wa haraka, wale waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo ambao wanapokea matibabu.

Ajali hiyo inadaiwa kusababishwa na lori lililopoteza mwelekeo na kugonga matatu iliyokuwa ikiwasafirisha mahujaji hao.

Share This Article