Timu ya Kenya ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 Junior Starlets itaondoka nchini Jumatatu kuelekea Uhispania, kwa kambi ya wiki mbili kujiandaa kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa nchini Morocco kuanzia tarehe 17 mwezi huu.
Starlets inayofunzwa na kocha Mildred Omari imekuwa kambini kwa takriban mwezi mmoja katika uwanja wa Kasarani.
Wakiwa Uhispania Starlets watacheza mechi za kirafiki nchini Uhispania dhidi ya Australia,na vlabu vya Cadiz CF na Real Betis.
Kenya itaondoka uhispania siku mbili kabla ya mechi ya ufunguzi ya kundi E ya kombe la dunia dhidi ya Uchina Oktoba 17, kabla ya kumenyana na Marekani tarehe 22 na kuhitimsiha rativa dhidi ya Samoa Oktoba 25.