Rais Ruto akamilisha utoaji hatimiliki 300,000 Pwani

Ruto amesema kuwa hatimiliki hizo zitahakikisha wakazi wanaishi bila hofu ya kutimuliwa kutoka kwa makazi yao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amekamilisha zoezi la wiki moja la utoaji hatimiliki za ardhi 300,000 katika eneo la Pwani.

Rais amekamilisha zoezi hilo siku ya Jumamosi kwa kutoa hatimiliki 4,500 mjini Garsen, kaunti ya Tana River.

Jumla ya hatimiliki laki tatu zimetolewa kwa wamiliki wa ardhi katika eneo la Pwani ndani ya kipindi cha siku nane ambazo Rais Ruto amekuwa eneo hilo.

Ruto amesema kuwa hatimiliki hizo zitahakikisha wakazi wanaishi bila hofu ya kutimuliwa kutoka kwa makazi yao.

Aliongeza kuwa serikali inadhamiria kutoa hatimiliki nusu milioni kufikia mwezi Disemba mwaka huu na pia itanunua ardhi kutoka kwa wastawishaji wa kibinasfi ikiwemo ekari kumi kutoka kwa Wachu na kiasi sawa na hicho kutoa kwa Haganda na ekari zingine 5,000 kila moja kutoka kwa Kibusu na Kitangale ili kuwagawia maskwota.

Aliahidi kurejea eneo hilo na kutoa hatimiliki zingine laki mbili ndani ya kipindi cha miezi miwili ili kumaliza tatizo la uskwota katika eneo la Pwani.

Share This Article