Lori lakamatwa likisafirisha lita 10,000 za Ethanol Kiambu

Kulingana na maafisa, kemikali hiyo ilikuwa ikipelekwa kwenye kiwanda kimoja cha utengenezaji pombe Jijini Nairobi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Lori lakamatwa likisafirisha Ethanol kiambu.

Maafisa wa Polisi kaunti ya Kiambu, wamenasa lori lililokuwa likisafirisha lita 10,000 za kemikali aina ya Ethano, kwenye Barabara Kuu ya Nairobi-Nakuru.

Kulingana na maafisa, kemikali hiyo ilikuwa ikipelekwa kwenye kiwanda kimoja cha utengenezaji pombe Jijini Nairobi.

Watu watatu waliokuwa wakisafiri ndani ya lori hilo walikamatwa wakati wa operesheni hiyo, iliyotekelezwa na maafisa wa polisi kutoka Makao Makuu ya kaunti ndogo ya Lari.

Kamishna wa kaunti ya Kiambu George Matundura, aliyethibitisha kukamatwa kwa lori hilo, alisema washukiwa hao wanatarajiwa kuwasaidia polisi kwa uchunguzi, kubaini kemikali hiyo ilikotoka na ilikokuwa ikipelekwa.

Sampuli za kemikali hiyo zimepelekwa katika maabara ya serikali kwa uchunguzi.

Matundura alisema iwapo kemikali hiyo ingetumika kutengeneza pombe haramu, mapato yake yangekuwa takriban shilingi milioni 28.

TAGGED:
Share This Article