Viongozi wa ufalme wa Tooro nchini Uganda wanapanga urejesho wa mwili wa mfalme wao nchini humo.
wakiongozwa na waziri mkuu Calvin Armstrong Rwomiire Akiiki, pamoja na naibu wake, Henry Basaliza Mutegeki, wanaripotiwa kufanya mkutano wa faragha kwa muda katika makazi ya marehemu Mfalme Oyo huko Buziga hii leo.
Waziri Mkuu anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu mipango ya kurejesha mwili wa marehemu Mfalme Oyo katika Ufalme wa Tooro kwa ajili ya mazishi.
Ikumbukwe kwamba Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliagiza kwamba Mfalme Oyo aandaliwe mazishi rasmi na kwamba aliacha mrithi atakayetangazwa baadaye.
Huku hayo yakiiri, mwanamfalme mkuu wa ufalme wa Tooro aitwaye Charles Kamurasi Akiiki, amekanusha madai kwamba marehemu Mfalme Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi IV aliacha mtoto wa kurithi kiti cha enzi.
Kamurasi, ambaye ni Omusuuga na mkuu wa ukoo wa kifalme wa Babiito, alisema Familia ya Kifalme haikuwa na taarifa yoyote kuhusu mrithi huyo anayedaiwa kuwepo.
“Mfalme hakuwa na mtoto. Sifahamu kuhusu jambo hilo kwa sababu hatujawahi kuambiwa hivyo,” alisema Kamurasi.
Msimamo wake ni kinyume na taarifa zilizotolewa na Waziri Mkuu wa Tooro, Calvin Armstrong Rwomiire Akiiki, pamoja na Rais Yoweri Museveni.