Washukiwa 14 wanaohusishwa na msururu wa uhalifu wa mtandaoni mjini Nakuru wamekamatwa.
Washukiwa hao walikamatwa wakati wa operesheni iliyofanywa na wapelelezi kutoka Kitengo cha Upelelezi wa Ulaghai wa Benki (BFIU) na maafisa kutoka kituo cha polisi cha Nakuru.
Operesheni hiyo ilifanywa katika eneo la Pangani mjini Nakuru ambapo washukiwa walipatikana chumbani wakiendesha shughuli zao za udukuzi.
Simu 25 na kadi za simu ni miongoni mwa vitu vilivyopatikana wakati wa operesheni hiyo.
Uchunguzi ulifichua kuwa washukiwa hao walibuni tovuti bandia ikiwa ni pamoja na za Zain Coach, Harmain Coach, na Habesh Coach, wanazotumia kuwaibia wasafiri wasiokuwa na habari ya shughuli zao.
Washukiwa kwa sasa wanaandikisha taarifa wakisubiri kufikishwa mahakamani.