Helikopta ya watalii yaanguka Samburu

Hatima ya waliokuwamo bado haijabainika huku timu ya uokozi ikiripotiwa kuelekea eneo la ajali hiyo.

Martin Mwanje
0 Min Read
Mlima Ololokwe

Helikopta ya watalii imeripotiwa kuanguka karibu na Mlima Ololokwe katika kaunti ya Samburu.

Hatima ya waliokuwamo bado haijabainika.

Helikopta hiyo yenye makao yake katika eneo la Loisaba iliripotiwa kuwachukua watalii kutoka kambi ya Suiyan.

Timu ya uokozi inasemekana kuelekea eneo la ajali hiyo, ingawa maelezo ya kina kuhusu ajali hiyo bado hayajabainika.

Tutakupa maelezo zaidi punde tukipata taarifa. 

 

Share This Article