Kenya Police FC ndio mabingwa wa Ligi kuu ya FKF, msimu wa mwaka 2024/2025 kwa mara ya kwanza tangu wapandishwe ngazi mwaka 2021.
Police wametawazwa mabingwa kufuatia ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Shabana FC ,siku ya Jumapili katika uwanja wa Kenyatta kaunti ya Machakos.
Police wameshinda kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu wapandishwe ngazi kutoka ligi ya NSL mwaka 2021.
Gor Mahia wameilemea Ulinzi Stars mabao 3-2, ushindi ambao haukutosha kuwapa ubingwa wa 22.
Police wanaongoza jedwali kwa alama 64,pointi 6 zaidi ya Gor Mahia, wanaokalia nafasi ya pili.
Police wataiwakilisha Kenya katika kipute cha Ligi ya Mabingwa msimu ujao kwa mara ya kwanza.