Viongozi wa kisiasa wametakiwa kufanya kampeni za amani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Wito huo umetolewa wakati kuna ongezeko la machafuko ya mara kwa mara kwenye mikutano ya kisiasa nchini.
Akizungumza mjini Tala, mbunge wa Matungu Stephen Mule amelaani vikali matukio ya jana huko Homabay akitoa rai kwa kanisa kuwa mstari wa mbele kuwakemea wanasiasa wanaofadhili wahuni kuzua machafuko hayo.
Akieleza kwamba iwapo mtindo wa kutumia magenge ya wahuni kwenye mikutano ya amani ya siasa hautakoma, taifa litajipata kwenye ghasia za uchaguzi mwaka 2027.
Matamshi ya Mule yanajiri baada ya kushuhudiwa kwa ghasia katika kaunti ya Homa Bay kwenye mkutano wa siasa wa vuguvugu la Linda Mwananchi.
Taarifa ya Jonathan Musau