Wakenya wamehizwa kusitisha unyanyapaa na kutowabagua wanaougua afya ya akili.
Mbunge wa Dagoretti Kaskazini Beatrice Elachi, alisema unyanyapaa na ubaguzi vinasalia kikwazo kikuu katika utafutaji wa matibabu ya afya ya akili hapa nchini.
“Watu wengi wanatekesa kwa sababu uwoga na pia kutokana na habari potovu kuhusu afya ya akili,” alisema Elachi.
Mbunge huyo aliyasema hayo Alhamisi wakati wa mkutano kuhusu afya ya akili na utoaji mafunzo ya kiusalama kwa Chama cha Wabunge wa kike nchini Kenya (KEWOPA).
Kuligana na Elachi, viongozi wa kisiasa wanajukumu la kutekeleza katika kukabiliana na unyanyapaa kwa wale wanaokabiliwa na changamoto za afya ya akili.
“Tunapaswa kutokomeza dhana kwamba ugonjwa na akili ni kuwa wazimu kupitia elimu na kuwasaidia walio na chanagamoto za kiakili,” aliongeza Mbunge huyo.
KEWOPA ilishirikiana na wakfu wa NIVISHE kutoa mafunzo hayo kwa wabunge hao, ambao walielezea changamoto wanakumbana nazo kama wanawake kwenye siasa.
Wabunge hao walitoa wito wa mjadala wazi ili kufanya iwe kawaida kwa wanaokabiliwa na changamoto za akili kutafuta usaidizi.