Ebola yaenea katika mkoa wa sita nchini DRC

Shirika la Afya Duniani  (WHO), limesema ugonjwa huo unaenea kwa kasi sana kuliko maabukizi ya hapo awali.

Tom Mathinji
1 Min Read
Ebola yaenea katika mkoa wa sita nchini DRC.

Kituo cha kudhibiti na kuzia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC), kimesema ugonjwa wa Ebola umeenea katika mkoa wa sita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mkuu wa kituo hicho Jean Kaseya leo Alhamisi, amesema kifo kimeripotiwa katika eneo la Buta ambalo ni Makao Makuu ya mkoa wa Bas-Uele.

Kulingana na Kaseya, mtu huyo anadaiwa alisafiri kutoka mkoa wa Haut-Uele.

“Ikiwa hatutasitisha msambao huu, utadumu zaidi ya mwaka mmoja na utakuwa mkubwa zaidi duniani,” alionya Kaseya.

Shirika la Afya Duniani  (WHO), limesema ugonjwa huo unaenea kwa kasi sana kuliko maabukizi ya hapo awali.

Mlipuko huo ulianza katika mkoa wa Ituri, kabla ya kuenea katika mikoa ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, Haut-Uele na Tshopo.

Hadi sasa watu 2,128 wamefariki kati ya visa 4,566 vilivyonakiliwa, kulingana na takwimu za serikali.

Share This Article