Liangfeng: Kutoka kijiji kilichoharibiwa hadi kivutio cha utalii China

Ufufuaji wa vijijini umebadilisha mazingira na kuinua kipato cha wakazi wa Liangfeng.

KBC Digital News
2 Min Read

Chongqing:  Awali kikiwa eneo lililoathiriwa na uchimbaji wa makaa ya mawe, lenye nyumba zilizopasuka, ardhi iliyotitia na uoto mdogo wa mimea, Kijiji cha Liangfeng kimepitia mabadiliko makubwa na kuwa kijiji cha kitaifa muhimu cha utalii wa vijijini.

Kijiji hicho kilichoko katika mpaka wa Chongqing na Guizhou, ndani ya eneo la maendeleo ya kiuchumi la Wansheng, Liangfeng kinaongozwa na falsafa ya “Yu Gan Yu Xing”, kauli mbiu ya eneo hilo inayosisitiza imani kwamba uvumilivu na bidii hatimaye huleta ustawi. Wakazi wanasema falsafa hiyo imekuwa msingi wa safari ya maendeleo ya jamii hiyo kwa miaka mingi.

Kikiwa karibu na hifadhi ya misitu ya Jiuguoqing, kijiji hicho kimejenga maendeleo yake kwa kutumia utajiri wa mazingira yake ya asili. Tangu Machi 2017, takwwinu zinainyesha kuwa kimepokea zaidi ya wageni milioni 3 na kupata mapato ya zaidi ya yuan milioni 600, sawa na takribani dola za Marekani milioni 84, kutokana na utalii.

Tangu kuanzishwa kwa mkakati wa China wa kufufua maendeleo ya vijijini mwaka 2017, Liangfeng imeendeleza utalii wa mazingira, uvuvi wa burudani na masoko ya bidhaa za kilimo zinazozalishwa nchini. Utalii pia umechochea ukuaji wa nyumba za kulala wageni na biashara nyingine ndogo ndogo, na hivyo kuwaletea wakazi fursa mpya za kiuchumi huku wakihifadhi mazingira ya asili ya eneo hilo.

Uamsho wa kijiji hicho unaakisi mabadiliko mapana zaidi yaliyofanyika Wansheng, eneo lenye historia ya zaidi ya miaka 180 ya uchimbaji wa makaa ya mawe. Wastani wa mapato ya kila mwaka yanayoweza kutumiwa na kaya huko Liangfeng umeongezeka kutoka yuan 6,000 hadi yuan 28,900, huku uchumi wa pamoja wa kijiji ukizalisha zaidi ya yuan milioni 1.5 kwa mwaka kutokana na shughuli zake.

Leo, wageni huja Liangfeng si kwa ajili ya kufurahia mandhari pekee, bali pia kushuhudia jamii ambayo ufufuaji wa maendeleo ya vijijini unaonekana katika maisha ya kila siku, kuanzia biashara zinazoendeshwa na familia na bidhaa za kilimo za eneo hilo hadi uchumi wa utalii unaoendelea kunawiri

Kwa hisani ya iChongqing.info

Share This Article