Huzuni yatanda Turkana wakati wa mazishi ya mwanafunzi wa Utumishi Girls

radiotaifa
1 Min Read

Vilio na majonzi vilitanda katika kijiji cha Towokayeni, eneo la Kakuma katika kaunti ya Turkana, wakati wa hafla ya mazishi ya mwanafunzi wa Gredi ya 10, Fortune Aimaya Losike.

Fortune ni mmoja wa wanafunzi 16 waliofariki kutokana na mkasa wa moto uliotokea Mei 28 katika shule ya Utumishi Girls Academy mjini Gilgil, kaunti ya Nakuru.

Alifariki alipokuwa akiwaokoa wenzake waliokuwa wamezungukwa na moto bwenini.

Waombolezaji walifurika nyumbani kwao mjini Kakuma ambapo walimkumbuka Fortune kama mwanafunzi aliyetia bidii ya mchwa masomoni na mwenye heshima.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria mazishi hayo waliitaka serikali kuchunguza chanzo cha moto huo na kufidia familia zote 16 zilizofiwa.

Taarifa ya mwanahabari wetu Philip Ekadeli

Share This Article