Mkenya Kelvin Kimtai anyakua dhahabu ya pili Ghana

Kelvin Loti Kimtai, alipiga kasi katika mita 100 za mwisho na kuishindia Kenya dhahabu ya mita 800,akizikamilisha kwa dakika 1 sekunde 45.47.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya ilinyakua nishani ya dhahabu ya pili katika siku ya tatu ya mashindano ya Riadha Barani Afrika, mjini Accra, Ghana, siku ya Alhamisi.

Kelvin Loti Kimtai, alipiga kasi katika mita 100 za mwisho na kuishindia Kenya dhahabu ya mita 800,akizikamilisha kwa dakika 1 sekunde 45.47.

Imade Boucheda wa Morocco, aliyekuwa akiongoza kwa kipindi kirefu alishinda fedha kwa dakika 1 sekunde 45.62, huku Alex Amankwah ,wa Ghana, akiridhia shaba.

Hata hivyo matumaini ya Kenya kushinda medali katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji wanaume, yaliyeyuka baada ya Shadrack Kibiwot kumaliza wa nne.

Godana Gemechu kutoka Ethiopia, alishinda dhahabu ,fedha ikamwendea Salahendinne Benyazzid wa Morocco, wakati Samuel Ferehew wa Ethiopia akiambulia shaba.

Mashindano hayo yataingia siku ya nne leo wakenya wakishiriki katika fainali ya mita 10,000 wanawake.

Kufikia sasa Kenya imenyakua dhahabu 2 fedha 1 na shaba 2.

Share This Article