David Keter wa chama tawala cha UDA, amechaguliwa Mbunge mpya wa Emurua Dikirr, katika uchaguzi mdogo ulioandaliwa siku ya Alhamisi.
Keter alizoa jumla ya kura 18,266, alimbwaga mwaniaji wa chama cha Democracy for Citizens Party (DCP), Vincent Kibet Rotich, aliyepata kura 10,760 .
Matokeo ya kura hizo yametangazwa mapema Ijumaa katika kituo cha ujumuishaji kura cha Dikirr Technical Training Institute, na msimamizi wa uchaguzi huo Caleb Gikonde, baada ya kupokea matokeo ya vituo vyote 94.
UDA imehifadhi kiti hicho kilichoachwa wazi kufuatia kifo cha Johanna Ng’eno, mwezi Februari mwaka huu kwenye mkasa wa ajali ya ndege.