Mudavadi awasili Azerbaijan kwa kongamano la miji

Hii inafuatia kongano la miji barani Afrika, lililoandaliwa  baina ya Aprili 8 na 10 mwaka huu.

Dismas Otuke
1 Min Read
Musalia Mudavadi - Mkuu wa Mawaziri

Waziri aliye na mamlaka Musalia Mudavadi, amewasili mjini Baku,Azerbaijan, kuhudhuria kongamano la 13 la miji Duniani kati ya Mei 17 na 22.

Mudavadi anatarajiwa kufanya maandalizi ya ziara ya Rais William Ruto, ambaye ataongoza ujumbe wa serikali ya Kenya kwenye kongamano hilo.

Kongamano hilo linaandaliwa kwa kauliumbiu“Housing the world: Safe and resilient cities and communities”.
Viongozi kutoka mataifa mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo la siku tano.

Hii inafuatia kongano la miji barani Afrika, lililoandaliwa  baina ya Aprili 8 na 10 mwaka huu.

Share This Article