Kaunti ya Bungoma imekabiliwa na ongezeko la visa vya uhalifu katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Kamanda wa polisi kaunti ya Bungoma Francis Kooli akitoa takwimu za visa vya uhalifu mwaka 2023 na 2024, aliwataka wananchi kuwa katika mstari wa mbele kukomesha uhalifu.
Kooli alisema kuwa uhalifu ambao umetekelezwa kwa kiwngi kikubwa katika kaunti hiyo ni pamoja na mauaji, ubakaji, na uvamizi.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, kulikuwa na mauaji ya 57 mwaka jana ikilinganishwa na mwaka 2003, ambapo watu 62 waliuawa, eneo la Webuye East likiwa na idadi kubwa ya waliouawa, ikiwa 15, ikifuatwa na Kimilili na Bungoma South.
Visa vya ubakaji na unajisi pia vilipungua mwaka jana hadi 248 kutoka 262 vilivyoripotiwa mwaka 2023, huku visa vya uvamizi 847 vikinakiliwa mwaka jana pekee.
Kooli amesema hatalegeza kamba katika juhudi za kudumisha usalama na kuitaka jamii ya eneo hilo kutatua mizozo kwa majadiliano badala ya vita huku akiwahimiza wazazi kuwachunga watoto wao kutokana na watu waovu.