EAC na SADC kukutana Tanzania kuhusu hali DRC

Dismas Otuke
1 Min Read
Watu watoroka makwao katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Kongamano lisilo la kawaida la pamoja baina ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kujadili hali ya usalama mjini Goma, limeratibiwa kuandaliwa kati ya Ijumaa na Jumamosi hii mjini Dar es Salaam, Tanzania.

Hii inafuatia makubaliano kati ya mwenyekiti wa SADC ambaye pia ni Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa na mwenyekiti wa EAC, Rais William Ruto wa Kenya.

Kulingana na taarifa hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, amekubali kuandaa kongamano hilo huku Marais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) na Paul Kagame wa Rwanda, wakitoa ithibati kushiriki.

Vile vile, Rais Ruto amethibitisha kuwa amejadiliana na Marais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Yoweri Museveni wa Uganda, na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, huku wote wakitoa ithibati kuhudhuria kongamano hilo lisilo la kawaida.

Website |  + posts
Share This Article