Mtandao wa afisi ya msajili wa mashirika wadukuliwa yasema Wizara ya Habari

Dismas Otuke
1 Min Read
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali, William Kabogo.

Wizara ya Habari na Uchumi dijitali imeanzisha uchuguzi kuhusu kudukuliwa kwa mtandao wa afisi ya msajili mkuu wa mashirika (BSR).

Kulingana na taarifa ya Waziri wa Habari na Uchumi dijitali William Kabogo, wamechukua tahadhari inayofaa kuzuia matumizi mabaya ya data ilikusanywa na wadukuzi hao na kuomba umma kuwa makini dhidi ya kupotoshwa.

Wizara hiyo pia imeweka mikakati tosha ya usalama wa mitandaoni kuzuia hali hiyi kutokea tena siku zijazo.

Kabogo amewataka Wakenya kuripoti visa vyovyote vinavyokisiwa kuwa udukuzi ili kulinda taarifa muhimu na kutotapeliwa mitandaoni.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *