Kenya na Korea Kusini zinaimarisha juhudi za kuboresha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji, kwa manufaa ya nchi hizo mbili.
Rais William Ruto amesema kuwa Kenya inadhamini uhusiano wa kidiplomasia na Korea Kusini, ambao alisema unaboresha ushirikiano wa nchi hizo mbili.
“Tunaimarisha ushirikiano wetu wa katika sekta za biashara, uwekezaji, elimu, sayansi na utengenezaji bidhaa,” alisema Rais Ruto.
Kiongozi huyo wa taifa alisema ili kubuni fursa zaidi za kibiashara kati ya nchi hizo mbili, wanashirikiana kuondoa vizingiti vinavyozuia bidhaa za kilimo kutoka Kenya kuingia Korea Kusini.
Aliyasema hayo Alhamisi, alipokutana na Spika wa Bunge la Taifa la Korea Kusini Woo Won-shik, katika Ikulu ya Nairobi.