Gabriel Martinelli alilipiga bao la jioni katika dakika 95 na kuwanusuru mabingwa mara tano wa dunia Brazi kuwabwaga Japani na kufuzu kwa raundi ya 16 bora ya Kombe la Dunia mwaka huu.
Japani ukipenda Samurai Blue, walichukua uongozi kunako kipindi cha kwanza dakika ya 29 kupitia kwa mshambulizi Kaishu Sano na kuongoza hadi mapumziko uwanjani Houston, Marekani Jumatatu usiku.
Casemiro aliwakomboa vijana wa Carlo Ancelotti kunako dakika ya 56, akiunganisha pasi ya Gabriel kwa goli la kusawazisha.
Mechi ikikaribia kumalizika na timu zikijiandaa kwa dakika 30 za ziada, Bruno Guimaraes alipata pasi murwa na kumkabidhi Martinelli na bila kusita akatikisa nyavu.