Ufaransa ilihitaji penalti ya dakika ya 70 iliyofungwa na nahodha Kylian Mbappe ili kushinda Paraguay bao moja bila na kujikatia tiketi kwa robo fainali ya Kombe la Dunia.
Paraguay walikaa ngumu katika mechi hiyo ya Jumamosi usiku katika uwanja wa Philadelphia na kuzima mashambulizi yote ya The Blues ya Ufaransa, wakionekana kutaka kusukuma mechi kwa muda wa ziada.
Hata hivyo, penalti hiyo haikuwavunja moyo Paraguay bali walijikaza kisabuni wakishindwa kwa bao hilo moja kufikia kipenga cha mwisho.
Ufaransa yake Didier Deschamps itakutana na wawakilishi wa Afrika, Morocco Julai 9 mjini Boston katika robo fainali ya kwanza.
Morocco iliwachakaza Canada magoli 3-0 katika mchuano wa kwanza wa raundi ya 16 bora Jumamosi jioni.