Timu mbili zitakazochuana katika robo fainali ya pili zitabainika Jumapili usiku katika siku ya pili ya mechi za awamu ya 16.
Mabingwa mara tano Brazil, Samba Boys, watakabiliana na Norway katika uwanja wa New Jersey kaunzia saa tano usiku kabla ya El Tri ya Mexico kuwaalika Three Lions ya Uingereza katika uchanjaa wa Mexico City saa tisa alfajiri Jumatatu.
Washindi wa mechi za Jumapili wataweka miadi ya kumenyana kwenye robo fainali ya Julai 10.